Data yangu italindwaje ninapotumia mfumo wa kuripoti wa mtandaoni?
Kanuni za ulinzi wa data – mfumo wa kuripoti wa mtandaoni
Ulinzi wa data ni muhimu kwetu
Tunachukulia suala la ulinzi wa data yako ya binafsi kwa uzito sana. Taarifa ifuatayo ya faragha ya data itakufahamisha kuhusu data ya binafsi tunayochakata unapotembelea tovuti hii au unaporipoti tukio la ukiukaji wa kanuni.
1. Mdhibiti wa data ndani ya ufafanuzi wa Kifungu cha 4 nambari 7 cha GDPR
Mdhibiti wa data anayechakata data ndani ya ufafanuzi wa Kifungu cha 4 nambari 7 cha GDPR ni mpokeaji wa data unayeonyeshwa unaporipoti tukio la ukiukaji wa kanuni.
2. Kuripoti matukio ya ukiukaji wa kanuni kupitia mfumo wa kuripoti wa mtandaoni/Kuwasiliana na Timu ya Utiifu
Kusudi la uchakataji wa data na msingi wa kisheria
Mfumo huu wa kuripoti wa mtandaoni ulisanidiwa kwa ajili ya kuripoti masuala yanayohusiana na utiifu. Unaweza kuutumia kuripoti matukio yanayoweza kukiuka kanuni za utiifu ambayo yanaweza kusababisha athari kubwa kwa kampuni, ikijumuisha adhabu za uhalifu au faini za usimamizi.
Unaweza pia kutumia mfumo wa kuripoti wa mtandaoni ikiwa una maswali maalum kuhusu masuala ya utiifu ambayo ungependa yajibiwe na timu ya Utiifu.
Msingi wa kisheria wa uchakataji huu wa data ni Kifungu cha 6 (1) sentensi ya 1 f) cha GDPR.
Aina ya data inayochakatwa
Ni hiari yako kutumia mfumo wa kuripoti wa mtandaoni. Data tunayochakata inategemea maelezo unayotupatia. Kwa kawaida tunachakata data ifuatayo:
- Jina na maelezo yako ya mawasiliano, ikiwa umetupatia maelezo haya.
- Iwapo wewe ni mfanyakazi wetu au la, ikiwa ungependa kutujulisha.
- Majina ya watu na data nyingine ya binafsi inayohusiana na mtu, kulingana na suala unaloripoti kwetu.
Wapokeaji/Aina za wapokeaji
Data unayotutumia huchakatwa na mdhibiti wa data na ndani idara ya Utiifu pekee. Kama kanuni, haturuhusu utoaji wowote wa data kwa watu wengine. Huenda ikawa kwamba tunahitaji kushiriki data uliyotutumia na idara zingine ndani ya shirika linalodhibiti data au na kampuni nyingine za Schwarz Group ikiwa ni muhimu ili kuchunguza suala husika.
Data pia huchakatwa kwa niaba yetu na wachakataji, kama vile msimamizi wa mfumo huu wa kuripoti wa mtandaoni, EQS Group GmbH, Bayreuther Strasse 35, 10789 Berlin, Ujerumani. Mchakataji huyu na wachakataji wengine wowote huchaguliwa kwa makini, na pia hukaguliwa na kuunganishwa na mkataba kwa mujibu wa Kifungu cha 28 cha GDPR.
Tunawajibika kisheria kumfahamisha mshtakiwa kwamba tumepokea ripoti kumhusu mradi hatua hiyo ya kumfahamisha haihatarishi tena uchunguzi wa ripoti husika. Hata hivyo, utambulisho wako kama mtoboa siri haufichuliwi kwa mtu ambaye anadaiwa kutekeleza tukio la ukiukaji wa kanuni, kwa kiwango ambacho hatua hii inaruhusiwa kisheria.
Kipindi cha uhifadhi/Vigezo vya kubainisha kipindi cha uhifadhi
Data huhifadhiwa kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo ili kutimiza makusudi yaliyotajwa awali, ambayo ni kufanya uchunguzi wa ripoti na kutekeleza hatua ya kuripoti kwa usiri kuhusu hali na chanzo cha ripoti husika na njia ya mawasiliano iliyotumiwa kuripoti, na kama inavyohitajika chini ya sheria husika. Vigezo vinavyobainisha kipindi hiki inajumuisha utata wa suala lililoripotiwa, muda unaochukuliwa kulichunguza na suala kuu la madai hayo. Data hufutwa baada ya kusudi la ukusanyaji kukamilishwa.
3. Matumizi ya mfumo wa kuripoti wa mtandaoni
Mawasiliano kati ya kifaa chako na mfumo wa kuripoti wa mtandaoni hufanyika kupitia muunganisho uliosimbwa kwa njia fiche (SSL). Anwani yako ya IP haihifadhiwi. Kidakuzi kilicho na kitambulisho cha kipindi (kidakuzi cha kipindi) huhifadhiwa kwenye kompyuta yako kwa madhumuni maalum ya kudumisha muunganisho kwenye mfumo wa kuripoti wa mtandaoni. Kidakuzi hiki hutumika kwa muda wa kipindi chako kisha hufutwa.
4. Haki zako kama mmiliki wa data
Una haki, kwa mujibu wa Kifungu cha 15 (1) cha GDPR, baada ya kuomba, kupokea maelezo bila malipo kuhusu data yako ya binafsi ambayo imehifadhiwa kwenye mfumo wa mdhibiti wa data.
Ukitimiza masharti ya kisheria, una pia haki ya kurekebisha, kufuta na kuzuia uchakataji wa data yako ya binafsi.
Ikiwa data imechakatwa kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) e) au f) cha GDPR, una haki ya kupinga. Ukipinga uchakataji wa data, haitachakatwa baadaye isipokuwa mdhibiti wa data aweze kuthibitisha misingi thabiti ya kisheria ya kuchakatawa zaidi ambayo inazidi maslahi ya mmiliki wa data.
Ikiwa umetoa data mwenyewe, una haki ya kuihamishia kwa mtu mwingine.
Ikiwa data imechakatwa kwa msingi wa idhini yako kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) a) au cha 9 (2) a) cha GDPR, unaweza kuondoa idhini yako wakati wowote kwa uchakataji wa baadaye bila kuathiri uhalali wa uchakataji wa awali.
Katika hali zilizotajwa hapo juu, ikiwa una maswali yoyote zaidi au ungependa kuwasilisha malalamiko, tafadhali wasiliana na Afisa wetu wa Ulinzi wa Data kwa barua au kwa barua pepe; angalia sehemu ya 5.
Una pia haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka yanayofaa ya usimamizi wa ulinzi wa data.
5. Wasiliana na afisa wa ulinzi wa data
Ikiwa una maswali yoyote zaidi kuhusu uchakataji wa data yako au utekelezaji wa haki zako, unaweza kuwasiliana na afisa wa ulinzi wa data wa mdhibiti husika:
- Kaufland Stiftung & Co. KG
z.Hd. Datenschutzbeauftragter
Rötelstraße 35
74172 Neckarsulm
Ujerumani
datenschutz@kaufland.com
- ”Кауфланд България ЕООД енд Ко“ КД
Ул. „Скопие“ 1А
София 1233
България
dataprotection@kaufland.bg
- Kaufland Romania SCS
Str. Barbu-Vacarescu 120-144
Sect.2. Bucuresti
România
protectiadatelor@kaufland.ro
- Kaufland Hrvatska k.d.
Službenik za zaštitu podataka
Donje Svetice 14
10 000 Zagreb
Hrvatska
Barua pepe: gdpr@kaufland.hr
- Kaufland Česká republika v.o.s.
Právo a Compliance
Bělohorská 2428/203
169 00 Praha 6
Jamhuri ya Zechia
oou@kaufland.cz
- Kaufland Slovenská republika v.o.s.
Právo a Compliance
Adresa: Trnavská cesta 41/A, 831 04 Bratislava
Slovakia
dataprotection@kaufland.sk
- Kaufland Polska Markety sp. z o.o. sp. k.
Al. Armii Krajowej 47
50-541 Wrocław
Polandi
daneosobowe@kaufland.pl